Tuesday, June 11, 2013

KUFUNDISHA MTOTO

Mama: "Mwanangu,njoo nikufundishe hesabu.." 

Dogo: "Haya mama." 

Mama: "Kwa mfano shangazi yako akikupa maandazi mawili, halafu akakupa tena maandazi mawili jibu lako litakuwa nini?" 

Dogo: "Asante shangazi."

MUUZA SAMAKI NA MTEJA


Mteja; Samaki bei gani?

Muuzaji; 2500.

Mteja; Mwisho?

Muuzaji; Mkiani.

Mteja; Mbona samaki mwenyewe kalegea?

Muuzaji; Labda alikua shoga baharini.