Tuesday, October 8, 2013

JIPANGE..USIKURUPUKE

Mshikaji kakosana na mpenzi wake, wamenuniana kama siku tatu hivi, mshikaji anaishi Tabata, binti anaishi Ukonga. 

Siku ya tatu jamaa akaamua amtumie SMS binti ya kumuomba msamaha yaishe warudiane. 

Akatuma SMS 

"Mpenzi kwa kweli nimekosa, nimejirudi naomba nisamehe yaishe". 

Akakaa kama dakika tano hajajibiwa SMS, akatuma ya pili. 

Akasubiri kama dakika kumi, hakuna jibu, akatuma ya tatu, ya nne na ya tano, zote kimya. 

Jamaa kwa hasira akaona binti anamdharau, akamwandikia SMS nyingine, 

"Ujue we mwanamke bwege sana, uzuri wenyewe huna, shepu hovyo, resepsheni ya kuunga unga, na bora tuachane tu, ndo maana natoka na rafiki yako Anna ananipa kila aina ya raha". 

Akaa kama dakika tano akaona kimya, akaamua apige amtukane vizuri, ile kupiga simu ikapokelewa na mtu mwingine akamwambia jamaa: 

"Kaka samahani huyu dada kaacha simu hapa kwenye chaji ametoka kama nusu saa imepita, ndo nampelekea simu kwake". 

Mshikaji akapagawa, akaanza: 

"Samahani naomba futa meseji ya mwisho niliyoituma please, nipe namba yako nikutumie hela, naomba unisaidie ndugu yangu!" . 

JIPANGE kabla hujaamua!

No comments:

Post a Comment