MKAKA: Mambo mrembo?
MDADA: Safi
MKAKA: Tafadhali naomba nizungumze machache na wewe
MDADA: We vipi kila mwanamke ukimuona unataka kuongea nae
MKAKA: Nisikilize kwanza, mi mtu mzima nina akili zangu siwezi kukusimamisha bila sababu
MDADA: Ok unasemaje?
MKAKA: Asante kwa kunipa muda, mimi ni GM hapo benki, ndugu zangu wamekuwa wakinilazimisha nioe nimekataa muda mrefu, nilipokuona tu roho imenisimama, nataka kukuoa basi
MDADA: Umesema GM wa Benki?
MKAKA: Ndio mrembo wangu nimekuwa GM hapo mwaka wa tatu sasa
MDADA: Wooow, hata mimi najiona muda wa kuolewa umefika, kuolewa na GM itanihakikishia maisha ya uhakika na mimi nitakutunza mume wangu, njoo nyumbani wakujue
MKAKA: Basi tufanye kesho, ili niombe ruksa kwa wakubwa waniruhusu kesho niwe off
MDADA: Kuomba ruksa kwa wakubwa? Mbona sikuelewei? We si ndio GM?
MKAKA: Ndio mimi GM yaani Gate Man sasa lazima niombe ruksa au nitapoteza kazi
MDADA: Mshenzi mkubwa unanipotezea muda wangu, najua naongea na mtu wa maana kumbe mfungua geti kwandraaa zako
No comments:
Post a Comment