LIFE BEGINS AT 40! So how old are you?
Huo ni msemo wanao waingereza.
Today is your future kwa taarifa yako.. Ulipokuwa mdogo ulisema nikiwa mkubwa nitakuwa na gari na nyumba nzuri wazazi wangu wataishi hivi na vile. Je unayo? Je imetokea? Maybe yes. But maybe no.
Kama haijatokea je bado hujawa mkubwa? Basi kama ni mkubwa ujue kuna kitu hujafanya.
Utasema tena nikifika miaka 40 nataka niwe na hiki na kile watoto wangu wasome international skul nk. Subiri uone miaka inavyoenda. Usishangae kufika 40 bado umeajiriwa kwa mtu na anakugombeza kwa nini mwanao anaumwa kila siku unachelewa kazini. Kazi nyingi. No bright future. No enjoyable present. Just existing and not living!
Hapo ndo unawaza kufuga ng'ombe wa maziwa kibamba kwenye kiwanja chako cha miguu 12 kwa 15! Wenzako wa umri wako hapo unasikia wameanzisha bness in Australia. Wamenunua kiwanja Mbezi Beach kwa 300M! Wanamiliki Apartment Johannesburg. Wakienda UK wanaenda kula The Ritz (Google that). Wanasomesha watoto zao the finest schools available wewe wa kwako wakati huo wamekosa nafasi Makongo wameenda Kibamba Secondary School wanapanda daladala sita kwenda na kurudi full kutukanwa na makonda.
Wenzako in their 40s wanasaidia wasio na uwezo katika jamii wewe ndo kwanza ukipokea simu kutoka kijijini una-mute! Wenzako in their 40s wakisikia kuna ujenzi wa nyumba ya ibada wanachangia 5M kimyakimya.. Wewe ukitoa laki moja basi mpaka mtaa wa saba watakujua! Halafu unashangaa wanazidi kuinuliwa. Mwenye nacho ataongezewa au hujui? Na asiye nacho..... (Malizia)
Wenzako in their 40s wana exposure ya uhakika. Walishafika kuanzia Sauzi, Botswana, Mozambique, Kenya, Ethiopia, Ghana, Naija, mpaka Egypt, The UK, Australia, Hawaii, Mexico, Croatia, The Netherlands, Switzerland, US, Panama mpaka Puerto Rico, Brazil na jirani zake, Hong Kong, Australia, Japan, China, (Incredible) India, Thailand, Singapore, New Zealand, Comorros, you name it..!! Wewe hata Kampala hujawahi fika. Kila siku Tegeta Posta ndo ruti yako miaka 15 mfululizo eti unatafutia watoto maisha! Unaishi au unaisha?
Acha mawazo mgando. Hiyo ajira ifanye serious sana tu lakini kwa muda tu. Jiandae kusimama mwenyewe. Kwani hujiamini? Na Mungu naye humwamini? Changamoto ni sehemu tu ya kufika kileleni. Don't be afraid. Don't dwell in that comfort zone!! Unasubiri kiinua mgongo? Utaenda kukiinvest wapi na kwa nguvu ipi. Na utaenjoy retirement kweli kama at 60 yrs ndo unafungua duka la vifaa vya ujenzi eti vinalipa. Kwa nini hukufungua ukiwa 30 ili uone vinalipa au la. At 60? With due respect.
Suffer the pain of discipline now. Or else you will suffer the pain of REGRET. Halafu ukianza kuregret ndo pressure zinakuja, stress, nk mwisho unawacha hata hao watoto in a far worse situation than your own lifetime.
Life Begins at 40 my friend.. How Old Are You?
No comments:
Post a Comment