Friday, October 26, 2012

MAMBO YA EID

Machizi watatu waliamua kuenda picnic milimani wapate view nzuri ya jiji, ili washerehekee pia na sikukuu hii ya Eid.

Ilipofika wakati wa kula wakatandika mkeka wao chini na kuweka misosi kwenye mkeka,hapo ndipo wakagundua wamesahau opener ya soda.

Wakakubaliana mmoja wao ashuke mlima, arudi nyumbani akachukue opener.


Yule aliyetumwa akasema,"Msije mkaanza kula wakati mi sipo!"



Wenziwe waka ahidi watamsubiri.



Basi akaondoka.

Ikapita saa ya kwanza jamaa hajarudi.

Saa ya pili kimya!

Saa ya tatu ikawa bado hajarudi, wenziwe wakajiuliza mbona nyumbani sio mbali hivo yaani mpaka sasa hajarudi,





wakaendelea kungoja huku njaa zikizidi kuwauma, lakini walivumilia, lisaa la nne likapita mpaka la tano na hapo giza likawa limeanza kuingia. 








wakaamua wafungue chakula waanze kula.

Walipoanza kula tu, yule chizi aliyetumwa akajitokeza, (alikuwa kajificha nyuma ya kichaka) akasema,





"Pumbavu nyie!! Unaona...nilijua tu mnataka kuninyima...haya basi mi siendi sasa!"



No comments:

Post a Comment