Simu ya binti inaita ngriiiiiiiiiii ngriiiiiiiiiii. Binti anapokea. Jamaa upande wa pili akaanza:
Jamaa: Haloo mpenzi, vipi hali yako?
Binti: Kichwa kinanigonga si mchezo, sijui ni maleria au ni kichwa tu! Naumwa sana. Uko wapi swirii?
Jamaa: Niko town my dear. Natamani nije kukuona baadaye, nikuletee nini?
Binti: Wow! Mpenzi unanipenda sana. Niletee Chipsi Kuku, Ice Cream, Chocolate, na lile gauni na viatu ulivyoniambia, na vocha ya buku 10 please!
Jamaa: Nilikuwa najua unaumwa ila naona uongo umekuzidi.
Binti: Khaa, naumwa mwenzio! Tena sana. Kwani vipi we mwanaume?!
Jamaa: Na mbona hiyo list ya vitu umetaja hakuna hata Panadol?!
Binti: Jamani, ni kujisahau tu mpenzi wangu!
Jamaa: Hauko serious! Chapa mwendo.
No comments:
Post a Comment