MSICHANA: Namchukia mvulana wangu.
ZUZU: Kwa nini?
MSICHANA: Yaani ni mtu wa bei rahisi sana, hawezi hata kuninunulia dinner. Hivi wanaume wote mpo hivyo?
ZUZU: Hapana. huyo yeye tu, sisi hatupo namna hiyo. Hata mimi sipo namna hiyo.
MSICHANA: Nakwenda kuachana nae leo hii hii.
ZUZU: Sawa. Ila utakapoachana nae, unaweza kuja kwangu, sina msichana halafu nakuhitaji sana.
MSICHANA: (Akasimama na kutaka kuondoka, ZUZU akamshika mkono)
ZUZU: Ndio unataka kuondoka? Unakwendawapi sasa?
MSICHANA: Nakwenda kuvunja uhusiano na yeye ili niwe nawe kwa uhuru.
ZUZU: Hapana. Huwezi kuondoka.
MSICHANA: Kwa nini?
ZUZU: Sasa ukiondoka nani atakayelipia hiki chakula tulichokula!
No comments:
Post a Comment