Thursday, August 22, 2013

BARUA YA WAZI KWA BILL GATES


Kwenda kwa: Bill Gates, Microsoft
Kutoka kwa: Zuzu, Tanzania
Tarehe: 22 Agosti 2013 ...
...

YAH: MATATIZO KWENYE COMPUTER YETU.
Ndugu Bill Gates,
Anko wangu amenunua kompyuta mpya kwa ajili ya kutumia nyumbani kwetu. Nilipoichunguza nimegundua ina matatizo kadhaa.
Nimeamua kukuandikia barua hii ili uyafanyie kazi.

1. Kuna batani ya 'start' lakini hakuna batani ya 'stop'. Tafadhali tazama kwa makini.

2. Nina mashaka kama umeweka 're-guta' maana nimeona umeweka tu 're-cycle', lakini nyumbani kwetu kuna guta na siyo baskeli.

3. Pia nimeona kuna sehemu ya 'Find' lakini wala haifanyi kazi. Anti yangu jana alipoteza funguo.
Nimejaribu sana kubonyeza find ili itusaidie kutafuta funguo imeshindwa. Naripoti tatizo hili.

4. Nimeona tu kuna 'Microsoft word' sasa nataka kujifunza 'Microsoft sentence', sasa ni lini utatuwekea Microsoft Sentence?

5. Tumenunua CPU, mouse na keyboard, lakini kuna kipicha kimoja tu kinachoonyesha 'My Computer':
lini utatuwekea vipicha kwa ajili ya hivyo vifaa vingine?

6. Nimeshangaa kuona kompyuta imeandika mahali 'MY Pictures' lakini sijaona picha yangu hata moja humo. Lini mtaziweka?

7. Pia mmeweka 'MICROSOFT OFFICE' inakuwaje kuhusu 'MICROSOFT HOME' kwa kuwa hii ni kompyuta tunayotumia nyumbani
kwetu na wala siyo ofisini.

8. Pia umeweka 'My Recent Documents'. Vipi kuhusu 'My Past Documents'?

9. Pia umeweka 'My Network Places'. Tafadhali sana iondoe hiyo maana anko atakuwa anajua
mahali nilipo, kuna siku huwa natoroka shule.

Jambo la mwisho. Wewe jina lako ni GATES sasa kwa nini umeamua kuuza WINDOWS?

Wako mtiifu
ZUZU!


No comments:

Post a Comment