MWALIMU Kasinzia darasani , DOGO kamfuata na kumwambia Teacher mbona umetupa zoezi tufanye alafu unasinzia ??
[MWALIMU:] ''hapana mimi sijalala !"
[DOGO]: ''kwani hapa ulikuwa unafanya nini mda huu ? mimi nimekuona umelala''
[MWALIMU:] ''nilikuwa naongea na MUNGU!''
KESHO YAKE
DOGO kasinzia Darasana wakati kipindi linaendelea. MWALIMU akamuamsha
"DOGO, Yani unathubutu kusinzia kwenye kipindi changu?"
[DOGO:] "Hapana mwalimu sijasinzia!"
[MWALIMU:] " Enhee Tuambie Basi ulikuwa unafanya nini ? maana darasa zima limekuona"
[DOGO: ] "nilikuwa naongea na MUNGU na mimi Pia "
MWALIMU Kwa Hasira huku akipiga kelele , " Enhe Hebu Tuambie MUNGU wako Amesemaje ???!?!" maana naona watu mnatafuta Viboko Asubuhi Asubuhi.
[DOGO:] "MUNGU Kasema Hakuongea na wewe Hapo Jana !"
No comments:
Post a Comment