Mtu na mkewe walienda hospitali ili mke aweze kujifungua mtoto.
Walipofika daktari akawaambia ametengeneza mashine ambayo ina uwezo wa kuhamisha kiasi cha maumivu ya kuijfungua kutoka kwa mama kwenda kwa baba wa mtoto.
Basi jamaa kusikia hivyo akaomba kiasi cha maumivu ya uzazi kihamishwe kutoka kwa mkewe kwenda kwake. Dokta akakubali ili akamuonya jamaa kwamba maumivu ni makali kuliko maumivu ya aina yoyote ile ambayo amewahi kuyapata.
Jamaa akakubali.
Basi dokta akaenda kwenye mashine akabonyeza 90% ya maumivu kwa mama, 10% kwa baba.
Huku harakati za mama kujifungua mtoto zikiendelea jamaa akamwambia dokta:
najiskia niko fiti kabisa endelea kunihamishia hayo maumivu toka kwa mke wangu.
Dokta akaenda kwenye mashine akaongeza maumivu kwenda kwa baba hadi 20%.
Jamaa bado akawa anajiskia vizuri tu.
Dokta ikambidi ampime presha na mapigo ya moyo akaona kweli jamaa bado yuko fiti. Dokta akashangaa sana.
Kwa kuwa zoezi la kuhamisha maumivu toka kwa mama kwenda kwa baba lilikuwa linampa sana unafuu mama aliyekuwa anajifungua, mume mtu akamshauri dokta amuhamishie maumivu yote yeye.
Dokta akaenda kwenye mashine akakandamiza maumivu 100% yaenda kwa mwanaume na jamaa akawa bado yuko sawa kabisa.
Basi mama akajifungua mtoto mzuri tu wa kiume na jamaa na mkewe pamoja na baby boy wao wakarudi nyumbani. Ile kufika tu home wakamkuta house boy kaanguka getini kadedi kitambo
No comments:
Post a Comment