basi leo asubuhi nimemuona mrembo mzuri masikini hata hawezi kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!
Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa katikati ili akija nimpishe,
dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa kama ya kukatia vitunguu likaa!
Duh linanuka tu sigara,
Yule Mrembo akasimama, limoyo likauma kweli!,
Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka, aisee kama zali na Mrembo akakaa!
Jaman Bahati iliyoje,nikalianzisha,
MIMI : Mambo Mrembo.
MREMBO : poa,
MIMI : Karibu Karanga (nikatoa vinjugu vya kuzugia)
MREMBO : silagi huo Uchafu,labda Pop Corn na Clips.
MIMI : Ok naitwa Chogomundu Pangalashaba mwenzangu?
MREMBO : He he heee! Jina kama dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,
Wakati naendelea kupata majibu Machungu ghafla Nikaona Gari imefika Namanga, kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha ningeenda kushuka nae popote nikamwambia konda
"Shusha Namanga" ,
sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo hapo!
MIMI : haa kumbe na wewe unashuka hapa?
YEYE : so what?
MIMI : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama ntilie tukagonge chai,andazi maharage,
YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa natumia vitu kama Burger,Kuku, sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai, yaani Uzuri Wangu woote unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,
Dah Mrembo akasepa zake, nikaona hakuna Noma nikaagiza zangu Maharage ya 200,maandazi mawili
200 na Chai ya 100, nikaacha kajero hapo nikasepa,
Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.
SHANGAZI : mwanangu Chogomundu Karibu Baba!,
MIMI: asante Shangazi
SHANGAZI: yule mwanangu wa Mwisho unamkumbuka?
MIMI : Si yule Kipandauso?
SHANGAZI: huyo huyo!
MIMI : namjua vizuri,wakati anakuwa namuona,hata nepi nimembadili teh!, yupo wapi siku hizi?
SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi TRA pale karibu na ITV, ila yupo alienda Chuo akahisi homa kaona arudi,ngoja nimuite,
Kipandausooooo!!!
KIPANDAUSO : beeee Mama!
SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna Mgeni!
Hamad! Ndipo Macho yangu yakakutana na Yule Mrembo wa Kwenye daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena,muda huu komwe la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!,
mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa Mchele!,
Aliponiona Almanusura azimie!!!,
huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!,
ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!
SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha na kikombe kingine cha uji uje unywe na Kaka yako!
Dah! akarudi ndani kinoma noma kainamisha sura chini, mi nikawa najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger?
Wapi Sausage?, anyway bado nipo hapa kwa Shangazi mpaka baadae.
No comments:
Post a Comment