Saturday, May 24, 2014

MAANA YA SERIKALI

Mtoto mdogo alimfuata baba yake na kumuliza, " Nini maana ya SIASA?"

Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu kujibu kwa mfano huu: mimi natafuta fedha ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI

Mama yako yeye anasimamia matumizi ya fedha, hivyo mwite SERIKALI. 

Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie mahitaji yenu hivyo nyinyi twawaita WATU.

Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI. Na mdogo wako ambaye ni mdogo tunamwita FURSA ZA BAADAYE"

 Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone kama ina kupa jibu la kuridhisha.... 

Kijana akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri na kuyatafakari  maneno aliyoyasema baba.

Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua kuamka na kwenda kumcheki.

 Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada.

Akaamua aende chumbani kwa baba na mama, akamshuhudia mama akiwa peke yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote.

Hakutaka kumwamsha akaona angemsumbua mama, akarudi na kwenda shumba cha dada wa kazi na kuona mlango umefungwa. 

Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na kuona dada wa kazi akiwa na baba wanafanya yao. 

Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya kuwa na msaada wowote kwa mdogo wake.

Siku ya pili mtoto akamwambia baba,  "sasa nafikiri naelewa maana halisi ya SIASA."

Baba akasema, " safi sana mtoto mzuri, haya sasa niambie kwa maneno yako maana halisi ya siasa kwa jinsi ulivyoitafakari"

Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI anamyanyasa na kumtumia vibaya MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi mzito, Na WATU  hawasikilizwi shida zao huku FURSA ZA BAADAYE zikiwa  zimesusiwa kwenye uchafu bila msaada.

Baba kidogo azimie.

wewe ungejibu vipi?

No comments:

Post a Comment