Saturday, May 17, 2014

WASANII WATANO (5) MATAJIRI NCHINI

1. NASEEB ABDUL (DIAMOND)
Ni msanii aliye leta mapinduzi makubwa katika muziki hasahasa katika show za stejini yaani live performance .ni msanii anaye lipwa pesa nyingi kwa sasa tanzania kwa show moja anayo fanya. pia ni msanii mwenye show nyingi kwa mwezi kuliko wote,.hii imechangia kuweza kupata pesa nyingi katika mda mfupi.anamiliki nyumba kadhaa,viwanja,magari,maduka.

2. JOSEPH HAULE (PROFESSOR JAY)
Nguli wa muziki wa bongo fleva tanzania,anafanya show nyingi za nje,ni msanii aaliye dumu kwa mda mrefu,anamiliki nyumba ya kisasa ya zaidi ya tsh.mil 100, anamiliki gari,mashamba

3. JUDITH WAMBURA (LADY JAY DEE)
Ni msanii mwenye heshima sana tanzania kutokana na kujiheshimu kwake,kapata mafanikio sana katika kazi zake za muziki na kuweza kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine.kwani uchapa kazi wake ndo sababu ya mafanikio yake kimaisha.
Mali anazomiliki ni pamoja na -gari aina ya murano thamani ya
tsh.mil 45, basi aina ya costa tsh.mil.30, prado, nyumba nzuri ya kisasa,pamoja na mgahawa wa nyumbani longe wenye thamani ya zaidi ya tsh.mil.150 pia alianzisha maji yake ya jay dee ambayo baadaye yalizuiwa.

4. AMBWENE YESAYA (AY)
AY ni msanii mkimnya sana na huwa haweki mambo yake hadharani sana hasahasa ya maisha yake.lakini ni msanii mwenye pesa nyingi kutokana na kufanya show nyingi za kimataifa zinazo mpatia pesa nyingi.anamiliki magari,ana duka la ngua,pia ana nguo zake maalumu zenye nembo ya jina lake

5. KALEYA HUMORS (LIFE IS SHORT)
Ni mzushi mmoja ambaye anamiliki uongo mwingi na uzushi wa ajabu ajabu.
Mali anazomiliki ni pamoja na nyumba aliyopanga sasa ( sio mali yake) , blog www.kaleyahumors.blogspot.com ambayo haijapata matangazo wala mtu anayemtembelea.

kujihakIkishia we tembelea blogu yake (www.kaleyahumors.blogspot.com)



Stori hii ni ya fix tupu 

No comments:

Post a Comment