NIKIKUMBUKA HUWA NACHEKA
SANA.
Nilipokuwa shule ya msingi kuanzia la 4 hadi la 7 maksi zangu za hesabu kwenye mitihani zilikuwa zinacheza kwenye 03%hadi 08%.Matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya darasa!
Yanapotangazwa mwalimu anaanza kuwaita wanafunzi kwa kuanzia maksi za chini kwenda juu (0-100), kwahiyo darasa lote linajua makaratasi yakiletwa lazima niitwe kama si wa kwanza basi wa pili.
Siku moja mwalimu akaanza kuita majina, mpaka akafikia kwenye maksi 30%, 40%, 50%, 60% ,70% bado tu mi hajaniita. Watu wakaanza kuniangalia waliokuwa karibu
wakaanza kuniuliza....
"" eeeh umepasua hujaitwa, ilikwaje??"
Nilianza kuvimba kichwa, huku mwalimu anaendelea kugawa tu makaratasi.
Yakabaki makaratasi ya waliopata 80%-90% bado mi sijaitwa tu.
Mara akabaki na karatasi moja mkononi, darasa lote macho kwangu hawaamini kinachotokea maana bado sijapata karatasi.
Mwishoni mwalimu akaangalia juu, kisha
akasema
"Kuna ng'ombe hajaandika jina kapata 0% aje achukue karatasi lake..."
No comments:
Post a Comment