Tuesday, October 28, 2014

MESEJI HAIKUFIKA

Mama mkwe kamkuta jamaa sebuleni kapandisha hasira anadai ataua mtu.

Mama Mkwe: Mwanangu kwani kuna nini jamani?

Jamaa: Leo namuua mwanao, mshenzi sana.

Mama Mkwe: Tulia jamani, kimetokea nini?

Jamaa: Mwanao mshenzi sana, nilikuwa nimesafiri, nikamtumia meseji kuwa nakuja, eti bado leo nimefika nimemkuta na mwanaume kwenye kitanda chetu, dharau gani hii, sikubali leo tunagawana majengo ya serikali, yeye anaenda kulala Muhimbili mi naenda kulala Segerea

Mama Mkwe: Subiri kwanza, mwanangu hayuko hivyo lazima kuna maelezo fulani kuhusu hili ngoja nimuulize...

mama mkwe akamfwata mwanawe na baada ya muda akarudi sebuleni.

Mama Mkwe: Unaona, nilijua mimi lazima kuna sababu. Kumbe mwenzio hakupata ile meseji uliyomtumia.

No comments:

Post a Comment