Saturday, December 8, 2012

BANGI HAIONGOPI.....

Mzee mmoja alikuwa anasumbua vijana waliokuwa wanavuta bangi nyuma ya nyumba yake na kuwatishia atawaitia polisi.

Siku moja wakati wale wavutaji bangi wanavuta vitu vyao wakapanga jinsi ya kumkomesha yule mzee ili asiwasumbue tena.

Mmoja wao akatoa wazo la kuisukuma nyumba ya yule mzee ili isonge mbali na eneo wanalovutia bangi...wote wakaunga mkono wazo hilo.


Wakavua mashati yao wakaanza kusukuma nyumba,wakati wanaisukuma yule mzee akapita akachukua mashati yao na kuyasongeza mbali bila wale wavuta bangi kumuona.

Walipochoka kusukuma,wakageuka kuchukua mashati yao walipo ona yako mbali na ile nyumba....wakaanza kupongezana,"Lo! Leo tumefanya kazi kweli...kesho tutaendelea kuisukuma mpaka itoke mtaani kwetu!!"



No comments:

Post a Comment