Bosi mmoja alikuwa na mazoea ya kununua wine anakunywa kidogo anaiacha juu ya kabati kisha anaenda kazini...lakini kila siku houseboy wake alieitwa Bakari alikuwa anakunywa kidogo alafu anaweka maji ili bosi asijue imepungua.
Bosi alihisi hali hii coz ilikuwa akiinywa tena baadae anakuta imebadilika ladha,siku moja akamuekea mtego kwa kununua wine ambayo ikiwekwa maji inabadili rangi na kuwa kama maziwa.
Kama kawaida bosi akanywa wine kidogo akaenda kazini,houseboy nae akaenda kama kawaida yake akanywa kidogo alafu akaweka maji...ghafla ikabilika rangi na kuwa kama maziwa...houseboy akachanganyikiwa akaenda kujificha jikoni.
Bosi aliporudi akakuta wine imebadilika rangi,akaanza kufoka,akamuita mke wake karibu na kumwambia leo tumeshika mwizi.
Bosi:"Bakari...wee Bakari!"
Bakari:"Yes boss."
Bosi:"kwanini umekunywa wine wangu na ukaweka maji?
Bakari:[Kimya]
Bosi:"Kwanini umekunywa wine yangu?"
Bakari:[Kimya]
Bosi akapandwa na hasira akamfuata bakari jikoni huku mkewe akiwa nyuma.
Bosi:"Nimekuita umeitika,lakini swali langu hujibu kwanini?
Bakari:"Bosi ukiwa huku jikoni hausikii kitu chochote isipokua jina lako tu,kama huamini baki humu ndani ujionee.
Bakari akatoka nje na mke wa bosi na kumwacha bosi ndani.
Bakari:"Boss."
Bosi:"Yes Bakari."
Bakari:"Nani hupenda kuingia chumba cha housegal wakati madam boss yuko kazini?"
Boss:[Kimya]
Bakari:"Nani hulala na housegal wakati madam boss amesafiri?"
Boss:[Kimya]
Bosi akafungua mlango wa jikoni,akatoka na kusema:"Walai maajabu ukiwa humu ndani huskii chochote isipokuwa jina lako tu!"
Mke wa bosi akaja juu:"Pumbavu! Waongo wakubwa nyie...nini kinaendelea hapa enh??"
Bakari:"Ukweli mama ukiwa ndani unasikia jina lako pekee....kama unabishana ingia utaamini!"
Mke wa bosi akaingia jikoni na kumwacha mume wake na bakari nje.
Bakari:"Madam?"
Mke:"Yes Bakari?"
Bakari:"Sema ukweli nani baba yake mtoto kati ya mimi na bosi?"
Mke:[Kimya]
Bakari:"Eeh..tuambie nani aliyekupa hio mimba?"
Mke:[Kimya]
Akafungua mlango akatoka:"Aaah...ni kweli,humu ndani kunahitaji maombi,yaani ukiwa ndani unasikia jina lako pekee!"
No comments:
Post a Comment