Tuesday, December 11, 2012

KASUKU MATATA

Mwanadada mmoja mrembo alienda mjini kufanya shopping,akapita mahali flani akaona muuzaji mmoja anauza kasuku elfu 25....akaamua kuulizia:

Dem:"Mambo."

Muuzaji:"Poa sista...nikusaidie nini?"


Dem:"Nilikuwa naulizia tuh...inaonekana huyu kasuku wako ni special maana unamuuza kwa bei ghali!"

Muuzaji:"Huyu kasuku huongea ndio maana namuuza kwa hio bei."

Yule dem akaamua kumjaribu pale pale...akamuuliza kasuku, "Mmmh..hebu niambie leo nakaaje?...mi najiona nimetoklezea!"

Kasuku akajibu:"Unaonekana kama MALAYA..."

Dem akakasirika na kusema,"Siwezi kumnunua kasuku huyu maana ni mshenzi ana tabia mbaya na za kipumbavu!!"

Muuzaji akamwambia yule dada asubiri kiasi...akamchukua kasuku na kuenda nae nyuma ya duka,akamzamisha ndani ya beseni lililojaa maji kwa dakika kadhaa...kisha akamtoa na kumwambia,"Pumbavu ukirudia kuongea ushenzi mbele ya wateja kama yule dada nitakuzamisha tena na safari hio hadi ufe...mshenzi wewee!!"

Aliporudi akamkuta yule mwanadada bado yupo akamwambia,"Dada samahani kwa tatizo hilo...naomba umuulize tena kasuku swali lolote."

Dem akauliza:"Nikirudi nyumbani kwangu na mwanamume mmoja utafikiriaje?"

Kasuku:"Kwa kweli nitafikiria huyo ni MUME WAKO."

Dem:"Nikirudi na wanaume wawili?"

Kasuku:"Hapo itakuwa MUME WAKO na KAKA YAKO."

Dem:"Je nikirudi nyumbani na wanaume watatu?"

Kasuku:"Hao watakuwa MUME WAKO,KAKA YAKE MUME WAKO na KAKA YAKO."

Dem:"Vipi je nikirudi nyumbani na wanaume wanne?"

Kasuku:"Aarggh!..Kudadeki!!! Lete hilo beseni la maji....nilishakwambia huyu dada ni MALAYA...!!!"

No comments:

Post a Comment