Siku moja nyani alikuwa kakaa kijiweni anavuta bangi,mjusi{Lizard} akaja akampa ''Hi." akamjoin na kumuomba puff.
Nyani akamuonya kuwa ile bangi ni kali,ni kipisi cha kutoka Ukunda.Mjuzi akapokea wakaanza kuvuta kwa raha zao,mjusi akawa hoi kwa stimu akamwambia nyani,"Duh,nasikia koo langu limekauka acha niende mtoni nikanywe maji."
Mjusi kufika mtoni kwa kuwa alikuwa na stimu nyingi akatumbukia mtoni.
Mamba aliyekuwa pembeni akawahi kumuokoa na kumtoa nje ya maji.
Mamba akamuuliza,"Inakuaje bro,mbona kutumbukia kwenye maji kizembe vile!!"
Mjusi akajibu,"Nilikuwa na Nyani tunavuta bangi nikasikia kui ya ajabu,nikajikuta kwenye maji bila kujua!"
Mamba akasema,"Wacha niende huko kwa nyani nikamuone."
Mamba kufika akamkuta nyani ndo anamaliza kile kipisi hata macho taabu kufungua.Mamba akamuita,"Oya!!"
Nyani akafungua macho kumuona mamba akashtuka,
"Duh! Mshikaji,kwani umekunywa maji yote mtoni...mbona umerudi mkubwa hivyo!!"
No comments:
Post a Comment