Kijana fulani alikuwa safarini, gari likamharibikia kijijini akaomba hifadhi katika nyumba moja akakaribishwa. Baada ya kuoga na kula:
Mzee mwenye nyumba: Sasa huyu mgeni sijui alale wapi?
Mama mwenye nyumba: Saa hizi ni usiku akalale na Bebi.
Jamaa kusikia jina Bebi akaona lazima huyu ni mtoto na labda anakojoa kitandani au analia akaona asije kumsumbua bure usiku.
Jamaa: Msipate tabu mi nitalala hapa hapa sebuleni kwenu.
Akalala.
Asubuhi wakati wanakunywa chai akaibuka msichana mmoja mrembo ajabu. Jamaa akapigwa na bumbuwazi karibu angejimwagia chai.
Binti: Umeamkaje mgeni? Naitwa Bebi, sijui wewe unaitwa nani?
Jamaa akajibu: aaaaaaaargghh!Mimi naitwa Mjinga bin Imekula Kwangu.
No comments:
Post a Comment