Wednesday, March 6, 2013

USHAURI

Mzee wa miaka 90 kaoa mke wa miaka 19. Baada ya muda mke apata ujauzito. 

Mzee akaenda kwa daktari kuomba ushauri. 

Mzee: Dokta, nina umri wa miaka 90 na sasa mke wangu mpya ni mjamzito. Na mlisema katika umri huu siwezi kumpa mwanamke ujauzito tena. Unaweza kunieleza chochote? 

Dokta: Labda nikupe mfano. Uko porini unawinda, ghafla ukamuona simba anakujia kwa kasi, ukanyanyua bunduki yako kumlenga simba umuue lakini ukagundua kwamba kumbe ulibeba mwamvuli badala ya bunduki, ghafla unamuona simba kaanguka na kufa kwa risasi. Utawaza nini? 

Mzee: Mhhhh, dokta hapo lazima kuna mtu mwingine porini muda huo ndo itakuwa kanisaidia kumpiga huyo simba risasi.

No comments:

Post a Comment