MAMBO 30 YANAYOKUONESHA KUWA SASA UMRI UMEKUTUPA MKONO....
1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi
2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani
3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe
4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini
5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala
6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa
7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club
8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei
9. Idadi ya tisheti na jinsi inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo
10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua
11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako
12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi
13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu
14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwapa mabaki uliyotoka nayo Subway ama Steers
15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana
16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala
17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulima lima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura
18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh' ngapi?"
19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba
20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Express, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani
21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati
22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"
23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati
24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa
25. Ukimwona rafiki yako yu mjamzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"
26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja
27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako
28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei na mfumo mbovu wa utawala
29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi
30. Ukimaliza kusoma kanuni hizo 29 hapo juu unaanza kuhesabu ambazo unaingia wewe.
Ukiona una nusu ya sifa hizi 30 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma.....!!!!!!!
No comments:
Post a Comment