Nimemkuta rafiki yangu analia kama mtoto mdogo chumbani kwake;
MIMI: Oya mshkaji vipi tena nani kafa?
MSHKAJI: Yaani Gulo kaniuwa, hivihivi bila kosa kaniuwa
MIMI: Hebu tulia nambie ishu nzima
MSHKAJI: Si unajua nimekuwa namlipia Gulo ada toka sekondari mpaka sasa yuko chuo nikijua ndio niko peke yangu na nitamuoa?
MIMI: Ndio
MSHKAJI: Jana nikataka kuangalia kanisevu nini kwenye simu yake
MIMI: Ok
MSHKAJI: Si kanisevu eti Mchungaji Peter 12
MIMI: Sasa tatizo liko wapi
MSHKAJI: Nilipoangalia majina mengine sinimekuta kuna Pasta Hamfrey, Pasta Henry, Askof Kitime , na kuna Mchungaji Peter 1 mpaka mimi wa 12, wakati hata siku moja haendi kanisani wala maombi
MIMI: Dah endelea kulia mwanangu
No comments:
Post a Comment