Saturday, March 23, 2013

MAMBO YA FORM FOUR

Moja ya sababu kwa nini asilimia 60 ya kizazi cha "Xaxa", "Xawa", "Xema", "Ya Ukwee" n.k. kimepata sufuri katika lipepa la form 4!

Haya ni baadhi ya majibu.


Pepa ya Maths.
Swali: Drake alinunua nyumba kwa mkopo was shilingi milioni 100 kwa riba ya asilimia 10 katika kipindi cha miaka miwili. Je atalipa shilingi ngapi jumla? (Maksi 10%)

Jibu: Mungu wangu! Umesema Drake wa Young Money Lebo? Kitu cha kwanza kabisa nipeni namba yake ya simu! Baada tu ya pepa nataka nipige naye kolabo!

Pepa ya Physics.

Swali: John hutumia dakika 40 kuendesha gari toka katikati ya mji hadi nyumbani kwake nahutumia mwendokasi wa kilomita 60 kwa saa. Kama angetembea kwa miguu angetumia mwendokasi gani kwa saa ili afike nyumbani kwa kutumia dakika 120?

Jibu: Kwanza kwa nini atumie miguu wakati gari analo? Mbona mnataka kututia wazimu? Atumie tu gari. Acheni hizi stori za kutumia miguu.

Pepa ya Bible:
Swali: David karudi nyumbani kutoka kazini na kumkuta mkewa amelala na mwanaume mwingine. Kulingana na maandiko ya Biblia na dhana nzima ya kusamehe, shauri huku ukitumia vifungu sahihi.

Jibu: Hapo hakuna stori. Vita lazima iwake! Mtu hawezi kula vitu vyangu namuangalia hivi hivi. Hamna mambo ya kifungu hata!

Pepa ya English:
Swali: Add a question tag on this sentence. "I am bored".
Jibu: Si uingie Facebook. Kuwega tag lazima uingie Facebook.


No comments:

Post a Comment