Sunday, May 19, 2013

BLENDA


Siku ya kwanza :
MUME: vipi mke wangu salama
MKE:salama tu mume wangu
MUME:uko wapi
MKE:niko nyumbani mume wangu
MUME:mmh kama kweli uko nyumbani hebu washa blender niisikie
mke akawasha blender - haya umeisikia ??
MUME:ndio mke wangu nimeiskia

Siku ya pili :
MUME:vipi mke wangu habari za hapo nyumbani
MKE:nzuri tu kamaulivyotuacha tuko poa 
MUME:uko wapi
MKE:niko nyumbani mume wangu
MUME:kama uko nyumbani hebu washa blender niisikie
mke akawasha blender - haya umeisikia ??
MUME:ndio mke wangu nimeisikia

siku ya tatu
mume akahamua kurudi bila taarifa around mchana akamkuta mfanyakazi nyumbani akamuuliza
 "vipi mbona uko peke yako mama yuko wapi ?"
 yule mfanyakazi akamwambia 
 "mama ameondoka na blender tokea asubuhi hajarudi ...."

No comments:

Post a Comment