Hapo zamani watu walikuwa wanamuona mtoa ... roho (Izraeli) anapokuja kuchukua roho zao.
Siku moja alienda kutoa roho ya jamaa mmoja aliyekuwa tapeli maarufu katika nchi ya misri.
Mtoa roho: "kwa mujibu wa listi yangu hapa inaonekana kuwa leo ndio siku yako ya kufa"
Tapeli: "enheeeee! nashukuru kweli maana nilikuwa naisubiri hiyo siku kwa hamu na nilikuwa nashangaa kwa nini unachelewa kuja"
Mtoa roho: "basi mshukuru mungu wako nimefika"
Tapeli: "Kwa furaha niliyo nayo naomba nikununulie hata soda au maziwa unywe halafu tuendelee na kutoa roho yangu"
Mtoa roho akakubali na kukaribishwa soda.
Kumbe yule tapeli akamtilia kilevi kikali katika soda, wakanywa wakaongea na kufurahi pamoja, kisha mtoa roho alipolewa na akalala
Tapeli akaichukua ile listi ya mtoa roho halafu akaliweka jina lake chini kabisa tokea kule juu.
Baada ya muda yule mtoa roho akaamka baada ya kilevi kile kumuisha
Mtoa roho: "Aisee kutokana na ukarimu uliouonyesha wa kunikaribisha kinywaji basi nitakupendelea ili usife leo
Tapeli: Kweli!?
Mtoa roho: "ndio, nilipokuwa nimelala niliongea na mungu na kumuomba ruhusa kuwa nisianzie juu kwenda chini katika orodha yangu badala yake nianzie chini kwenda juu ili uwe wa mwisho na mungu amenikubalia hivyo naomba listi
yangu katika begi nijue nani wa chini nianze naye"
No comments:
Post a Comment