Ilitokea hivi karibuni!
Kulikua na mabosi wawili wa kampuni moja ambao walikua wanapenda
sana kutoka pamoja hasa siku za mapumziko. Walikua wanawatumia madereva wao
kuwapeleka kila wanapoenda.
Kama ilivo kawaida kila bosi hujuana na dereva wake au boosi
kumjua vilivyo dereva wake. Siku moja, jumapili, wakiwa wametoka na kuelekea
maeneo ya ufukweni walianza kuzungumza na mazungumzo yakawa hivi:
Boss 1: aisee nakuambia sijawahi ona dereva mjinga kama huyu
niliyenaye!
Boss 2: aaaaah we waongea nini……….huwezi amini huyo dereva niliyenaye
yaani hamnazo kabisa.
Wakaendelea kubishana kila mmoja akisema dereva wake ni mjinga
zaidi ndipo ikabidi wathibitishe kwa kila mmoja kuonyesha ujinga wa dereva
wake.
Boss 1 akamuita dereva wake.
Boss 1: eeeeh chukua hii elfu 20 nenda kaninunulie FLAT TV inch 50 dukani!
Dereva: sawa boss, vp niilete huku au nipeleke nyumbani?
Boss 1: ukiweza kununua ilete hapa.
Dereva akaondoka, boss 1 akasema: waona alivo mjinga yaani hata
hajui kua kwa shilingi elfu 20 huwezi kupata FLAT TV INCH 50.
Wakacheka, Boss 2 akasema sasa ngoja umuone dereva wangu alivyo
mjinga.
Boss 2: hebu nenda nyumbani kaniangalie kama nipo!
Dereva: sawa bosi
Dereva akaondoka, Boss 2: waona alivyo mjinga, mimi nipo hapa
alafu ataenda nyumbani kuniangalia kama nipo
Wakacheka na kusema kweli huyu mjinga.
Upande wa pili wale madereva wakakutana na kuanza kuongea.
Dereva 1: huwezi amini sijawahi fanya kazi na Boss mjinga kama
huyu.
Dereva 2: bora wewe mi wangu ni punguani kabisa hata sijui
kapata wapi ubosi.
Dereva 1: sasa sikia kaniita sahivi ananiambia niende
nikamnunulie FLAT TV inch 50, wakati anajua fika kabisa kua leo ni jumapili na jioni hii
hakuna duka lililowazi kama sio ujinga ni nini??
Wakacheka!
Dereva 2: hahaha aisee ila hata hivyo hafikii kwa upunguani wa
bosi wangu, eti kaniita pale ananiambia niende nyumbani kwake nikamuangalie
kama yupo, ilhali anasimu pale angeweza tu kupiga kwa mkewe nyumbani amuulize
kama yupo au lah na sio kunisumbua mimi mpaka niende kwake naharibu mafuta tu...!!
Wakabaki wakicheka kila mmoja kuendelea na alichotumwa!
Je nani mjinga???? Mabosi au dereva??
No comments:
Post a Comment