Friday, April 13, 2012

WANAFUNZI WAONGO

Wanafunzi watano wa chuo kikuu kimoja hapa nchini walikuwa wanatakiwa wafanye mtihani siku inayofuata. Wale wanafunzi walikunywa pombe mpaka saa kumi za usiku,asubuhi ya siku ya mtihani kila mmoja alikuwa na uchovu wa Hangeover hivyo walishindwa kufanya mtihani.

Wakatunga uongo wa kwenda kumuongea Lecture wa somo husika. Wakaenda
kumuongopea Lecture kuwa wameshindwa kufanya mtihani kwa sababu jana walikuwa kwenye harusi na wakati wanarudi gari yao ikapata pancha na wakavamiwa na
vibaka na kuibiwa pamoja na kupigwa.

Yule Lecture alikubali na akawapa siku tatu za kujiweka sawa na kujiandaa na special exam. Siku ya mtihani wa Special yule Lecture aliwapa mtihani na aliwasimamia
mwenyewe.

Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama ifuatavyo,

1.Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano
2.Majibu yao lazima yawe sawa na yakiwa tofauti wote wanapata ziro na wanafeli 3.Mtihani huu una maswali matano na yote lazima yajibiwe.

Maswali ya mtihani yalikuwa hivi.

1.Harusi ilifanyika katika ukumbi gani?
2.Gari mliomtumia mpaka mkapata pancha inaitwaje?
3.Ajali imetokea eneo gani?
4.Nani alikuwa dereva?
5.Tairi ipi ilipata pancha,ya mbele au ya nyuma?

NAWATAKIA MTIHANI MWEMA

No comments:

Post a Comment