Thursday, November 8, 2012

BILA TAI


Kuna jamaa mmoja, Joti, alikua anatembea jangwani na kwa mda mrefu hakuona mji wala maji. Alikau amechoooka saana na ana kiu balaa. Kila akisogea mbele haoni mji wala sehemu yenye maji. Hakukata tama akaendelea kutembea japo kichovu sana. Kwa mbele mbaali akaona kama kijibanda akapata nguvu kidogo na kukaza mwendo.

Alipofika akamkuta jamaa kwenye kioski hicho anauza tai pekee. Hakuona dalili ya maji.

Muuzaji: karibu sana ujipatie tai maridhawa ambazo utavaa na kupendeza, tena kwa hiyo nguo yako hii itakupendeza saana, na kila mtu atakushangaa!.

Joti: (kwa hasira) yaani wewe mpuuzi kweli… mimi nina kiu ya maji na njaa nimechooka sana we unaniletea upumbavu wa tai saivi?? Mi nataka maji na chakula tu tai kale mwenyewe

Muuzaji: (akamjibu kwa sauti ya upole kabisa) "mimi nafanya hii biashara ya tai na ndio mana nikainadi bidhaa yangu, ila we ni mkorofi sana kama usingehitaji tai ungesema tu kawaida Kwamba huhitaji tai. Ila kukuonyesha Kwamba mimi ni muungwana nitakuonyesha na kukuelekeza wapi utapata unachohitaji."

Muuzaji akamuelekeza Joti

“ endelea kwenda mbele baada ya hiyo milima miwili, utakuta nyumba ya kaka yangu, ukifika apo utapata kila unachohitaji”

Joti akaondoka kwa nguvu akielekea alikoelekezwa.

Baaday ya masaa Matatu, Yule muuzaji akamuona Joti akirudi akiwa kachoka maradufu

Muuzaji: vp mwenzangu imekuaje umerudi tena, umefanikiwa??

Joti: (kwa sauti ya unyonge na uchovu uku aibu ikiwa tele) “nimefika kwa kaka yako ila yeye hauzi maji wala chakula, anatoa bure, lakini kila aingiaye nyumbani kwake lazima awe amevaa tai, hivyo nimekuja kununua tai”

No comments:

Post a Comment