Jamaa wawili
Mbongo na Mkenya waliomba kazi katika post moja katika shirika moja kubwa hapa nchini. Wote walikua na vigezo
sawa kwaio mkuu wa kitengo akasema kwakua kuna nafasi moja na nyie wote mna
vigezo sawa sasa itabidi niwape katest kidogo. Hivyo wakapewa kamtihani ka
kuandika.
Baada ya
kumaliza mtihani wote walipata maksi sawa na kulikosa swali moja katika kumi
(10).
Mkuu wa kitengo
akamfuata Mbongo na kumwambia,
“asante kwa
kuonyesha interest ya kutaka kufanya kazi katika kampuni yetu, lakini ni Kwamba
tumeamua kumpa kazi Mkenya”
Mbongo:
(akastuka)
“ kwanini iwe ivo il-hali wote tumepata maksi 9 sawa, hasa
ukizingatia hapa ni Tanzania na mimi ni Mtanzania nilistahili nipate hiyo
nafasi kwanini unampa mgeni??”
Mkuu wa
Kitengo:
“ni kweli wote mmepata maksi sawa, lakini uteuzi wetu haukutegemea
maswali mliyojibu sahihi bali umetokana na lile swali ambalo wote mmekosa”
Mbongo: “ sasa
apo ni kivipi majibu ya swali tulikosa, moja likawa afadhali kuliko lingine??”
Mkuu wa Kitengo:
“ rahisi sana,
swali la 5, Mkenya kajibu “SIJUI” na wewe umejibu “HATA MIMI””
No comments:
Post a Comment