Msichana wa miaka 16 alipata ujauzito. Wazazi wa binti walikasirika sana baada ya kugundua. Mama wa binti akaamua kumpa simu binti yake aongee na aliyempa mimba ili
akamfate aje naye.
Baada ya nusu saa binti aliondoka akarudi na mwanaume ambaye alioneka ni mzee wa makamo, huyo mzee alikuja na gari nyekundu nzuri sana akiwa na binti. Alipofika akaingia
ndani akawasalimia wazazi na kusema
"samahani sana wazazi kwani nimempa mimba binti yenu na sitomuoa, ila kama akijifungua mtoto wa kike nitawapa kiwanda kimoja, ghorofa moja na Tsh milioni mia mbili ila kama akijifungua mtoto wa kiume nitawapa viwanda viwili, ghorofa tatu na Tsh milioni mia tano, ila ikitokea mimba ikatoka sijui mngependa nifanyaje? (akawauliza wazazi wa binti)
baba wa binti akajibu
"apo itabidi umpe
mimba nyingine"
No comments:
Post a Comment