Tuesday, November 6, 2012

MAKOTI MAWILI

Joti aliamua kumtembelea rafiki yake Vengu ali ajue maendeleo ya ujenzi wa nyumba ya Vengu umefika wapi.

Alipofika akamkuta rafiki yake akitokwa na jasho jingi, huku akiwa bize anapaka nyumba rangi.

Joti alipomuangalia rafiki yake vizuri akagundua kuwa amevaa makoti mawili...akamuuliza:-

Joti: "Eee bwanae! Mbona makoti mawili na jua lote hili?"

Vengu: "Nataka hii kazi ya kupaka rangi itoke poa."

Joti: "Sa ndio uvae makoti mawili?"

Vengu: "Hasaa, (akachukua mkebe mmoja wa rangi na kumwonesha Joti)..Soma hapa."

Joti akasoma maandishi kwenye mkebe wa rangi:

"FOR BEST RESULTS PUT ON TWO COATS."

No comments:

Post a Comment