Nilienda kikazi Singida. Asbh mapema sna mm niko Ubungo nikapata tiketi ya dirishani. Muda kidogo akaja Jamaa kakaa pembeni yangu mm nikajua niko nae seat moja. Sasa mshangao ndo uliponianza:
Jamaa kaweka begi akatoa maji makubwa na keki mbili akala. Sikushangaa. Kufika Chalinze kanunua Mayai ya kuchemsha 3 na Hindi 1 la kuchemsha na Soda ya kopo (Fanta) akapiga taratiiibu!! Kufika Msamvu!! Kashuka karudi na Chipsi Mayai kanikuta nimekaa kwenye seat maana sikushuka. Gari halijaondoka kaita muuza korosho kanunua pakti kubwa huku kachukua machungwa 4. Mimi nikaanza kua na mashaka aisee!! Jamaa kapiga Taratibu!!
Tumeingia Dodoma saa saba hivi Heee!! Pale Four Ways watu tunashuka mchana tukafinye maana njaa sasa ilikua inauma Jamaa nae kashuka nikaguna MHH!!! Lahaula!! Jamaa kaingia Hotelini nae kaagiza Wali Samaki na Coca cola. Kwa kweli mimi nikaanza kumuogopa yule Jamaa!!! Nikaanza kufikiria mbona haombi kuchimba dawa?
Muda umefika gari linaondoka nikajua Jamaa lazima ataomba kuchimba dawa!! Lazima akakate GOGO!! Mhh!! Jamaa kainuka kavuta begi lake kapekua pekua karudisha kukaa namuona kashika Pande la muogo wa kuchoma na maji ya Kilimanjaro makubwa!! Kwenye mfuko wa shati kuna biskuti za chokleti. Nikainuka mbio mpaka kwa Dereva.
Niliogopa AISEE!!
Nikasema
"HIVI HUYU AKIJAMBA HUMU NDANI ITAKUAJE?"
Naombeni komenti zeni Jamani!!
Naombeni komenti zeni Jamani!!
No comments:
Post a Comment