Wednesday, November 14, 2012

SIMBA NA SUNGURA...

Hapo zamani kulikuwa na Chura aliyeishi pembezoni mwa Ziwa peke yake kwa miaka mingi.Alibahatika kupewa nguvu za kichawi na mchawi mmoja hivi.

Siku moja alibahatika kutoka nje ya Ziwa na kuona dunia ilivyokuwa poa,kitu chake cha kwanza kuona ilikuwa ni;Simba anamkumbiza Sungura,akapaza sauti na kuwaita wote waje,wakenda pale alipo.Kisha akawaambia,"Mimi ni Chura mwenye maajabu,kwa kuwa nyie ni wanyama wangu wa kwanza kuwaona,nitawapa nafasi ya kutimiza ndoto zenu leo,kila mtu achague vitu vita tu ambavyo angependa vitokee na mi nitampatia muda huu huu."

Simba Kwa kuwa alikuwa na tamaa akawa wa kwanza kutaja,"Ningependa kila SIMBA hapa msituni awe JIKE kasoro mimi tuh niwe DUME."...kulisikika sauti ya ajabu na ombi lake likawa kweli.


Zamu ya SUNGURA,"Mimi ningependa Helmeti kichwani." Ombi hili liliwachanganya wote Chura na Simba,lakini ndio hivyo...ikatokea sauti ajabu na Helmeti ikatokea kichwani mwa SUNGURA.

Zamu ya SIMBA tena,"Ningependa kila SIMBA katika misitu ya karibu na hapa tulipo awe JIKE."...kama kawaida sauti ya ajabu ikatokea na ikawa hivyo.

Zamu ya SUNGURA tena,"Mimi ningependa piki piki na iwe na mafuta full tanki!" Wote Simba na Chura wakawa wanashangaa,si angeomba pesa tu na angeweza nunua piki piki baadae...ikatokea sauti ya ajabu na pikipiki ikatokea.

Zamu ya SIMBA tena,"Ningependa SIMBA wote duniani wawe JIKE isipokuwa mimi tu."...ikatokea sauti ya ajabu na ikawa hivyo.

SUNGURA akacheka sana,akatupia Helmeti kichwani na kuwasha piki piki yake kisha akasema,"Ningependa SIMBA wote duniani wawe DUME,alafu huyu awe JIKE!!" na kutokaaa Ndukiiiii.



No comments:

Post a Comment