Mateja fresh wawili
walikuatana barabarani, mmoja akamshangaa mwenzie kumuona ana baiskeli nzuri
kweli na kwa uteja wao hakuweza kupata jibu jamaa kaipata wapi?
Hivyo akamuuliza,
TEJA
1: duh! Mwana bonge ya baiskeli, umeipata wapi?? Sidhani kama umenunua lazima
utakua umepora tu, ngoja wakudake?
TEJA 2:
aah mwanangu mwenyeeewee, sijanunua, sijaiba wala nini yaani?
TEJA
1: (kwa mshangao) hee! Sasa umeipata wap??
TEJA 2:
nilikua nakatiza kitaa cha beach, akaja mrembo mmoja wa ukweli anaeiendesha…. Akasimama
kasha akanicheeki akaitupa baiskeli chini na kuvua nguo zoote.. akajilaza chini
ananiambia.. "chukua chochote unachotaka.. hii ndo bahati yako zali la mentali".
TEJA
1: aah bora umechukua hiyo, maana kwa vyovyote nguo zake zisingekutosha
No comments:
Post a Comment