Wednesday, January 2, 2013

MPANGAJI MPYA

Mdada mmoja mrembo sana alikuwa kapewa talaka na mumewe akahamia nyumba aliyokuwa kapanga CHEKA..... 

CHEKA alipomuona mpangaji mpya roho yote ikamtoka... 

Akajitahidi kila njia kumuonyesha kuwa nae yupo na ni bachela, mdada akawa anaendelea na shughuli zake bila hata kuonyesha dalili za kumwona.... 

Jioni moja CHEKA akiwa kapumzika akasikia hodi kwenye chumba chake, alipofungua akakutana uso kwa uso na mdada mpangaji, kapendeza sana na akiwa kavaa kimini cha nguvu;


MDADA: "Samahani kaka, yaani nimekaa muda mrefu mpweke nimeona leo lazima nitoke nikajirushe kidogo kisha nipate bwana niondoe uchovu. Vipi we uko free?!?!"

CHEKA: "Aaaaah, mimi tena!!!! Mimi sana tu!!!! Niko free sina kitu chochote ninachofanya jioni hii, yaani niko free kabisaaaaaa, si unaona mwenyewe niko free sina ishu kabisaaa!!!! Tena hata mimi najisikia upweke upweke!!!!"

MDADA: "Loh!!!! Nakushukuru sana kaka yangu, basi ngoja nikuletee watoto wangu ushinde nao mpaka ntakaporudi!!!!"


No comments:

Post a Comment