MASANJA: niaje mrembo?
DA KIBOGA: we unaona aje?
MASANJA: nacheki umeiva ile sirias yaani...
DA KIBOGA: sasa juu ya hiyo unatakaje?
MASANJA: mmmmh... mi nataka tu tuwe mabeshte....
DA KIBOGA: kwani sahizi tupo kama maadui?
MASANJA: hahaha... sio hivyo, yaani, i mean tuwe closer than before...
DA KIBOGA: kwani sahizi tuko opener than before?
MASANJA: hehehe.. dah... si maanishi hivyo, i mean, nataka tuwe tunatembeleana... si unajua
DA KIBOGA: ati tunatembeleana? sasa kama viatu yako vina uchafu, ukinitembelea utanichafulia nguo... na kwanza ulivyo mzito, ukinitembelea nitavunjika na nipelekwe hospitali?
MASANJA: ai wewe... simaanishi hivyo, namaanisha tuwe tunaonana every now and then....
DA KIBOGA: sawa basi... ntakuletea picha yangu na wewe uniletee yako na uwe unaangalia yangu na mimi ntakua naangalia yako ... sawa?
MASANJA: yaani mimi ndo unanichezea akili hivyo kama mtoto? ...
DA KIBOGA: nimeichezea aje? si unaniona hapa? kwani nimeingia kwa kichwa chako?
MASANJA: acha hata niende... naona hatusaidiani.
DA KIBOGA: ulikua unataka tusaidiane kwani uliskia mimi ni member wa red cross au UN?
No comments:
Post a Comment