Wednesday, January 23, 2013

UWONGO WA SIMU

Mlevi alipanda daladala akiwa anatoka Msasani anaelekea kwake Ubungo, mara simu ya mdada jirani yake ikalia;

MDADA: Hellow, Sweety mambo? Niko kwenye daladala naelekea Kiwalani kwa shangazi kuna msiba ntakutafuta nikifika.

Baada ya muda simu ya mtu mwingine ikalia;


JAMAA: Hello, aise nivumilie hapa niko kwenye basi naelekea Ifakara nikirudi ntakupa mzigo wako. 

Simu ya konda ikalia,

KONDA: Vipi mshikaji, leo noma mwanangu, nimepata zali hapa napiga mzigo niko daladala la Mwenge Kunduchi.

MLEVI: (kwa sauti ya juu) Dereva!! simamisha gari nataka kushuka maana sijui hili gari linelekea wapi..

No comments:

Post a Comment