Saturday, January 5, 2013

TIKETI TAFADHALI


Maa ENGINEER watatu na WAHASIBU Watatu walikuwa wanasafiri kuelekea mkoani kwa kutumia TRENI , walikuwa wanaelekea mkoa Ambao treni ya TAZARA huishiaa , walipofika stesheni ya kupanda treni  WAHASIBU WATATU wali nunua tiketi kila mmoja na wale MA ENGENEER watatu walichanga pesa na kununua tiketi moja kwa ajili ya safari .

"Hivi kweli watu watatu wanaweza kusafiri kwa tiketi moja " aliuliza MUHASIBU mmoja 

ENGINEER mmoja alimujibu " tafadhali tazama utaona kama huamini MJINI shule kaka " .

Wote walipanda TRENI na kila mmoja ali kaaa katika Siti yake , Lakini Ma ENGENeer wao walizama katika Choo kilicho tazamani na SITi walio Kaa WAHASIBU .

Baada ya MUda Mfupi KONDAKTA alikuja kudai nauli , alichukua tiketi toka kwa wale WAHASIBU na kisha akagonga Mlango wa CHOO " ngo ngo ngo Ticketi tafadhali "

Mara mlango ukafunguka na mkono mmoja ulitoka na kutoa ticketi na konda anaichukua na kusepa zake .
"
WAHASIBU waliona yote yaliyo tendeka palee , walisema ni wazo zuri na lasaidia katika kusave nauli , baada ya majadiliano ya muda mfupi walikubaliana wafanye hivyoo wakiwa wanarudi DAr es laam .

Wakati wakurudi kama kawaida walifika stesheni na kununua tiketi Moja tuuh ya safari ya kurudi , walitoaa machoo baada ya kuona ma ENGENINEER safari hii hawakununua kitu kabisaa ...

"Hivi nyie Mta safiri Vipi , maana Hamna ticketi kabisaa ? " Aliuliza MUHASIBU mmoja hivi kati ya wale Watatu .

"Kijana tafadhali tazama na Utajioneaaa, walipo ingia ndani ya TRENI ma ENGNINEER wote watatu walizama Chooni na WAHASIBU nao wote Walizma CHoo cha Karibu Behewa lililo fuatia ...TRENI hiyoo ilianza SAFARII.

Muda Mfupi Baadae ENGINEER mmoja alichomoka toka chooni na kwenda katika choo kilicho kuwa na WAHASIBU ndani na ku gonga

" Ngoo ngoo ngooo TICKETI TAFADHALII "



No comments:

Post a Comment