Jamaa mmoja alikua anavuka boda (mpaka wa nchi moja kwenda nyingine) akiwa juu ya baiskeli na kabela viroba vya mchanga kushoto na kulia kama balance.
alipofika mpakani yule askari wa mpakani akamuuliza,
Askari: we! umebeba nini humo?
Jamaa: Mchanga
Askari: hebu shusha tuone na tukague, nyie ndo mwapitishaga magendo kwa staili hizi hizi mnaficha kwenye mchanga.
Jamaa: sawa unaweza pekua na kukagua
Askari akakagua na kukuta kweli ni mchanga, akamruhusu jamaa apite.
baada ya wiki mbili jamaa akapita tena akitaka kuvuka mpaka, yule askari akamkumbuka akamwambia shusha mzigo tuukague:
aliposhusha akagundua kweli ni mchanga akamruhusu.
hii ikawa inaendelea kila baada ya wiki mbili jamaa anapita pale kuingia iyo nchi na baiskeli na michanga.
siku moja yule askari akiwa hayupo kazini baada ya kustaafu, yupo mjini tu akamuona yule jamaa kwenye kisehemu akamfuata.
Askari: aisee vipi mzima wewe za siku?
Jamaa: aah salama, vp wewe?
Askari: niko mzima, sahivi nimestaafu, ila nina swali kidogo kwako.
jamaa: ok uliza tu
Askari: ujue miaka yote hiyo umekua ukipita na mchanga waingia huku nchini kwetu, nikikupekua unakua na mchanga, lakini bado nimekua nikihisi kuna magendo unafanya kuyaleta nchini ni nini hiko umekua ukikileta nchini? we nambie tu hii itakua siri yetu maana nimekua nikijiuliza sana pasipo kupata jibu, sitamwambia yoyote:
Jamaa akajibu " Baiskeli"
No comments:
Post a Comment