Joti siku hiyo baada ya kurudi hom usiku mkali wa manane akawa anajiandaa kwenda kulala, mkewe akamstua, hebu angalia kwa nje kule kwenye mwanga naona kuna kama vivuli vya watu. alipoangalia vizuri akagundua kuna wezi wameignia na wanafanya jaribio la kutaka kuiba kwake.
akainua simu taratiibu na kupiga Polisi masunzumzo yakawa hivi:
Joti: habari afande, nimevamiwa hapa nyumbani kwangu na wezi wanaiba tafandhali naomba msaada wenu.
Polisi: aisee pole sana nasikitika kukuambia kuwa hatutaweza kufika maana hapa kituoni hakuna hata mtu hivyo subiri wakipatikana tunatuma waje apo kwako.
Joti akajibu Poa kisha akakata simu.
baada ya dakika Moja Joti akapiga tena simu polisi akasema.
Joti: samahani afande ni mimi niliyepiga dk 1 iliyopita, msiwe na shaka hakuna haja ya kutuma maaskari, maana nimewapiga risasi na kuwauwa wezi wote.
kisha akakata simu.
hazikupita dakika 5 mapolisi na magari kama 6 ivi na ving'ora yakafika nyumbani kwa jamaa na kuwakamata wezi wote red-handed na ushahidi tosha na kuwaweka chini ya ulinzi na kuwapeleka lupango.
askari mmoja akamfuata joti na kumuuliza
Askari: aisee... imekuaje we si ulisema kwa simu kwamba umewaua wezi wote.. vp mbona tumekuta hivi??
Joti: aah mi mwenyewe nawashangaa nyie.. si mlisema hamna askari wa kuja kwangu??
No comments:
Post a Comment