Mzee: Umekuja kuposa huku unatafuna big g!!?
Jamaa: Natoa harufu ya sigara.
Mzee: Yani unavuta sigara!?
Jamaa: Vile nikitoka baa kulewa tu.
Mzee: yani Unalewa!?
Jamaa: Nilianza kulewa nilipokuwa jela.
Mzee: Yaani na kufungwa pia!?
Jamaa: Ah niliua mtu
Mzee: Duh kumbe wewe muuaji!?
Jamaa: Ah, si kuna mzee nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, mimi nikamuulia mbali.
Mzee: Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, mke mkeo uyu! Na mahali utaleta ukipata aina tabu..
CHEZEA KIFO WEWE!
No comments:
Post a Comment