Majamaa wawili Mpoki na Joti waliamua kwenda camping katika misitu flani kwa ajili ya kurefresh mind ana kupunguza stress.walipofika eneo la camp wakatengeneza hema lao na kwakuwa ilikua usiku tayari wakala na kisha wakalala ndani ya hema.
usiku mkali, Joti akashtuka toka usingizini akaangaza na kushangaaa..... akamuamsha Mpoki. Mpoki huwa anajifanya mjuaji sana.
Joti: we Mpoki amka kwanza
Mpoki: eeeh, vipi unasemaje?
Joti: hebu angalia Juu unaona nini?
Mpoki: aa naona nyota kama milioni hivi zikiwa zimetanda angani na kupendezesha anga
Joti: kwaio apo unapata picha gani au unaelewa nini?
Mpoki: apo inamaana anga iko tulivu na hakuna wingu la mvua wala dhoruba yoyote kwaio kuna usalama zaidi
Joti akamzaba bonge la kofi Mpoki, Mpoki akastuka...
Mpoki: sasa wanipiga nini??
Joti: Pumbaf yaani wajifanya unajuaa... hata hujagundua kuwa hema letu limeibiwa??
No comments:
Post a Comment