Saturday, October 5, 2013

MAMBO YA BOSI

Jamaa alikuwa akifanya kiwandani na kila siku alikua anafanya overtime. bosi wake akamuita na kumsifu na kumuahidi ya kwamba, kama akiendelea na moyo huo basi anamuhakikishia kumpa cheo kikubwa ofisini ndani ya muda mfupi na hata kumpatia hisa katika kampuni. 

jamaa akaongfeza bidii na masaa ya overtime.

Siku moja usiku akiwa katika overtime saa sita ya usiku TANESCO wakakata umeme, akaamua kutoroka na kurudi nyumbani kwake.

Alipofika nyumbani kwake akakuta gari la bosi wake limepaki nje, giza likiwa limetanda akazunguka kwenye dirisha la nyumba yake ili amgongee mkewe, alipogonga sauti ya bosi wake ilitoka chumbani kwake ikisema,

'Nani huyo?'

Jamaa akashtuka na kukimbia mbio kurudi kazini, akajisemea moyoni

' Dah nusura ningekamatwa na bosi'

No comments:

Post a Comment