Tuesday, May 27, 2014

DALILI ZA MTU MUONGO MUONGO

DALILI ZA MTU MUONGO MUONGO

1.Ukiona mtu anasema yupo veta anasomea biashara ujue kuna kitu

2.Ukiona mtu Kaandika yupo canada alafu ukikatika umeme mbagala anawatukana tanesco ujuekuna kitu

3.Ukiona mzee anasema enzi zangu shule nilikuwaga wa kwanza ujue kuna kitu

4.Ukiona mtu anasema wazungu wote matajiri ujue kuna kitu

5.Ukiona mtu anasema bakhresa alikuwaga shoe shine ujue kuna kitu

6.Ukiona msichana mwenye miaka zaidi ya 15 anaishi uswahilini alafu anasema mm bikra ujue kuna kitu

7.Ukiona mtu mwanaume anasema mm npo singo ujue kuna kitu

8.....

Nyingine ongeza ww

Monday, May 26, 2014

UKIKAMATWA NA POLISI

CHONDECHONDE UKIKAMATWA NA POLISI USITOE MAJIBU HAYA

Tafadhali ukiwa unaendesha gari ukasimamishwa  na 
polisi tafadhali jizuie usitumie majibu yafuatayo:
 
  • Hebu nishikie konyagi yangu nikutolee leseni 
  • Nilitaka na mimi kuwa polisi nikaona huu ufala
  • Unajua mshahara wako unatoka kwangu mimi mlipa kodi?
  • Bosi wako mwenyewe tulisoma nae praimari alikuwa mjingamjinga
  • Umejuaje nimekunywa, au na wewe mdau?
  • Jela zimetengenezwa kwa ajili yetu

METHALI MPYA

soma hizi methali mpya na wewe unipe yako moja

1. Simba mwendapole... Huyo ni Sharobaro
2. Asiyefunzwa na Mamae.. Ujue Mama hajapitia Ualimu
3. Zimwi likujualo.. Lilikuona Sehemu
4. Chelewa Chelewa.. Ukizikusanya utapata Ufagio
5. Hakuna Masika.. Wakati wa Kiangazi
6. Mpanda Ngazi.. atafika juu
7. Ukitaka cha Uvunguni.. Usishangae ukikuta ni Kichafu na vumbi
8. Hakuna Marefu.. Bila mafupi
9. Kuku Mgeni.. Hufungiwa mpaka azoee
10. Haba na haba.. Haba Mbili.
11. Penye wengi..Pana Ajali au Tukio hasa kigodoro
12. Ukiona vyaelea .. Ujue ni vyepesi

*** ENDELEZA ...!!?

WATCH TV

SPIK INGLISH

Saturday, May 24, 2014

MAANA YA SERIKALI

Mtoto mdogo alimfuata baba yake na kumuliza, " Nini maana ya SIASA?"

Baba akajibu, " Mwanangu ngoja nijaribu kujibu kwa mfano huu: mimi natafuta fedha ya matumizi, hivyo niite mimi BEPARI

Mama yako yeye anasimamia matumizi ya fedha, hivyo mwite SERIKALI. 

Mimi na mama yako tuko kwa ajili ya kuwapa nyie mahitaji yenu hivyo nyinyi twawaita WATU.

Dada wa kazi yeye anatusaidia kazi za hapa ndani hivyo tunamwita MFANYAKAZI. Na mdogo wako ambaye ni mdogo tunamwita FURSA ZA BAADAYE"

 Haya sasa mwanangu hebu fikiri na uone kama ina kupa jibu la kuridhisha.... 

Kijana akaondoka na kwenda kulala huku akifikiri na kuyatafakari  maneno aliyoyasema baba.

Baadae usiku ule, akasikia mtoto ambaye ni mdogo wake akiwa analia hivyo akaamua kuamka na kwenda kumcheki.

 Akaona mtoto kajinyea na kajipaka uchafu huo huku akilia kuashiria anahitaji msaada.

Akaamua aende chumbani kwa baba na mama, akamshuhudia mama akiwa peke yake kalala usingizi mzito na hana habari yoyote.

Hakutaka kumwamsha akaona angemsumbua mama, akarudi na kwenda shumba cha dada wa kazi na kuona mlango umefungwa. 

Akachungulia kupitia tundu la ufunguo na kuona dada wa kazi akiwa na baba wanafanya yao. 

Akakata tamaa na kurudi kulala bila ya kuwa na msaada wowote kwa mdogo wake.

Siku ya pili mtoto akamwambia baba,  "sasa nafikiri naelewa maana halisi ya SIASA."

Baba akasema, " safi sana mtoto mzuri, haya sasa niambie kwa maneno yako maana halisi ya siasa kwa jinsi ulivyoitafakari"

Mtoto akajibu, "Ni hivi, wakati BEPARI anamyanyasa na kumtumia vibaya MFANYAKAZI, SERIKALI imelala usingizi mzito, Na WATU  hawasikilizwi shida zao huku FURSA ZA BAADAYE zikiwa  zimesusiwa kwenye uchafu bila msaada.

Baba kidogo azimie.

wewe ungejibu vipi?

Thursday, May 22, 2014

HASIRA ZA KONDA

Konda alikuwa kakasirika sana, abiria alikuwa kagoma kulipa nauli akisisitiza eti yeye ni denti, wakati kila mtu alimuona ni mtu mzima, 

konda akamkunja jamaa, wakapigana sana, 

abiria alipoona anapigwa akaanza kukimbia, 

konda akamfukuza abiria akaaingia kwenye shimo, 

konda alipofika pale akakuta yeye hawezi kuingia kwenye shimo, kwa kisirani akaamua amkojolee humohumo kwenye shimo,

wananchi waliokuwa karibu wakamhamasisha konda, 

'Mnyee huyo, konda mnyee', 

konda akavua suruali na kulenga lile shimo na kuachia kitu. 

Hapo ndipo sauti ya hasira ya mkewe ikamuita, ikiambatana na makofi, konda akazinduka toka usingizini, akakuta kishaharibu mambo yote kitandani

WHO TOOK THE PHOTO???

LIE CLOCK

SHORTEST HORROR STORY

HOW IT FEELS

FREE OF CHARGE

The boss came early in the morning one day & found Andunje kissing his secretary.

He shouted at him, "Is this what I pay you for?"


Andunje replied: "No Sir, I do this free of charge"

GAMES

NO ONE WILL BUY

WOMEN... MULTITASKING

MAKE THE MOST OF WHAT YOU HAVE

Tuesday, May 20, 2014

KIPANDA USO

basi leo asubuhi nimemuona mrembo mzuri masikini hata hawezi kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko!

Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa katikati ili akija nimpishe,

dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa kama ya kukatia vitunguu likaa!

Duh linanuka tu sigara,

Yule Mrembo akasimama, limoyo likauma kweli!,

Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka, aisee kama zali na Mrembo akakaa!

Jaman Bahati iliyoje,nikalianzisha,

MIMI : Mambo Mrembo.
MREMBO : poa,
MIMI : Karibu Karanga (nikatoa vinjugu vya kuzugia)
MREMBO : silagi huo Uchafu,labda Pop Corn na Clips.
MIMI : Ok naitwa Chogomundu Pangalashaba mwenzangu?
MREMBO : He he heee! Jina kama dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,

Wakati naendelea kupata majibu Machungu ghafla Nikaona Gari imefika Namanga, kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha ningeenda kushuka nae popote nikamwambia konda

"Shusha Namanga" ,

sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo hapo!

MIMI : haa kumbe na wewe unashuka hapa?
YEYE : so what?
MIMI : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama ntilie tukagonge chai,andazi maharage,
YEYE : khaa! Unikome, mimi huwa natumia vitu kama Burger,Kuku, sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai, yaani Uzuri Wangu woote unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,

Dah Mrembo akasepa zake, nikaona hakuna Noma nikaagiza zangu Maharage ya 200,maandazi mawili
200 na Chai ya 100, nikaacha kajero hapo nikasepa,
Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.

SHANGAZI : mwanangu Chogomundu Karibu Baba!,
MIMI: asante Shangazi
SHANGAZI: yule mwanangu wa Mwisho unamkumbuka?
MIMI : Si yule Kipandauso?
SHANGAZI: huyo huyo!
MIMI : namjua vizuri,wakati anakuwa namuona,hata nepi nimembadili teh!, yupo wapi siku hizi?
SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi TRA pale karibu na ITV, ila yupo alienda Chuo akahisi homa kaona arudi,ngoja nimuite,
Kipandausooooo!!!
KIPANDAUSO : beeee Mama!
SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna Mgeni!

Hamad! Ndipo Macho yangu yakakutana na Yule Mrembo wa Kwenye daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena,muda huu komwe la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!,

mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa Mchele!,

Aliponiona Almanusura azimie!!!,

huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwisho wa Mjomba Dindoyogo!,

ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!

SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha na kikombe kingine cha uji uje unywe na Kaka yako!

Dah! akarudi ndani kinoma noma kainamisha sura chini, mi nikawa najiuliza wapi Pizza? Wapi Burger?
Wapi Sausage?, anyway bado nipo hapa kwa Shangazi mpaka baadae.

Saturday, May 17, 2014

WASANII WATANO (5) MATAJIRI NCHINI

1. NASEEB ABDUL (DIAMOND)
Ni msanii aliye leta mapinduzi makubwa katika muziki hasahasa katika show za stejini yaani live performance .ni msanii anaye lipwa pesa nyingi kwa sasa tanzania kwa show moja anayo fanya. pia ni msanii mwenye show nyingi kwa mwezi kuliko wote,.hii imechangia kuweza kupata pesa nyingi katika mda mfupi.anamiliki nyumba kadhaa,viwanja,magari,maduka.

2. JOSEPH HAULE (PROFESSOR JAY)
Nguli wa muziki wa bongo fleva tanzania,anafanya show nyingi za nje,ni msanii aaliye dumu kwa mda mrefu,anamiliki nyumba ya kisasa ya zaidi ya tsh.mil 100, anamiliki gari,mashamba

3. JUDITH WAMBURA (LADY JAY DEE)
Ni msanii mwenye heshima sana tanzania kutokana na kujiheshimu kwake,kapata mafanikio sana katika kazi zake za muziki na kuweza kuwa mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine.kwani uchapa kazi wake ndo sababu ya mafanikio yake kimaisha.
Mali anazomiliki ni pamoja na -gari aina ya murano thamani ya
tsh.mil 45, basi aina ya costa tsh.mil.30, prado, nyumba nzuri ya kisasa,pamoja na mgahawa wa nyumbani longe wenye thamani ya zaidi ya tsh.mil.150 pia alianzisha maji yake ya jay dee ambayo baadaye yalizuiwa.

4. AMBWENE YESAYA (AY)
AY ni msanii mkimnya sana na huwa haweki mambo yake hadharani sana hasahasa ya maisha yake.lakini ni msanii mwenye pesa nyingi kutokana na kufanya show nyingi za kimataifa zinazo mpatia pesa nyingi.anamiliki magari,ana duka la ngua,pia ana nguo zake maalumu zenye nembo ya jina lake

5. KALEYA HUMORS (LIFE IS SHORT)
Ni mzushi mmoja ambaye anamiliki uongo mwingi na uzushi wa ajabu ajabu.
Mali anazomiliki ni pamoja na nyumba aliyopanga sasa ( sio mali yake) , blog www.kaleyahumors.blogspot.com ambayo haijapata matangazo wala mtu anayemtembelea.

kujihakIkishia we tembelea blogu yake (www.kaleyahumors.blogspot.com)



Stori hii ni ya fix tupu 

BABA NI WEWE

MUME: Mke wangu, niwe mkweli pamoja na kuwa kwa sasa tuna watoto sita mimi bado nakupenda sana. Na hakuna kitu kitakachoweza kunifanya niache kukupenda, I love you honey. Nina swali moja tu, huyu mtoto wa nne mbona yuko tofauti na hawa wenzie sita, mkorofi, hataki shule yaani tabu tupu? Mke wangu nambie tu kama ana baba tofauti na wenzie, kiukweli halitabadili mapenzi yangu kwako.

MKE:(Huku akipiga magoti) Mume wangu najisikia vibaya naomba unisamehe ni kweli huyo mtoto baba yake ni tofauti na wenzie


MUME: (Machozi yakimlengalenga) Dah mke wangu... baba yake ni nani?


MKE: Baba yake ni wewe.

MTIHANI

WATEKAJI HOI

Eti majamaa wamemteka mtoto... Wakampigia mzazi... Wakamwambia.. tumemteka mtoto wako.. ili uweze kumpata itabidi utoe millioni kumi...

Yule mzee wala hakustuka... Akawauliza.. nashukuru sasa nafahamu mtoto wangu hajapotea bali mmemteka mko naye nyie...

Sasa je mnampa mahali pa kulala??

Majamaaa yakajibu.. ndio tena pazuri tu

Mzee akauliza. Vp mnampa chakula??

Majamaa yakajibu ndio tena kwa muda muafaka....

Mzee akawaambia...

Basi njooni maana kuna wadogo zake wanne muje muwachukue..mana mie hali ngumu kuwahudumia hawa wote ni taabu

JIWE

Siku moja Yesu alikuwa na wanafunzi wake nyikani,baada ya mafundisho marefu na jua kali wanafunzi wake walihisi njaa. 

Yesu alifahamu mawazo yao akasema, 

"Petro kalete jiwe", 

Petro alinyanyuka na baada ya muda alirudi akiwa na jiwe mkononi. Alipompa Yesu akalibariki likawa mkate, akawagawia wanafunzi wake wakala.

 Lakini hawakushiba, hivyo wakaanza kumlaumu Petro,..

"mbona umeleta jiwe dogo?", 

Petro akawajibu,

"me nilijua mwalimu anataka kukalia!".

Siku nyingine tena wakiwa nyikani, baada ya mafundisho marefu na jua kali, wanafunzi walihisi njaa. 


Yesu alifahamu mawazo yao,akasema

"Petro kalete jiwe". 

Basi walinyanyuka wanafunzi kama 6 hivi, wakaleta jiwe kubwa huku wakilibiringisha. 

Walipolifikisha Yesu alilikalia na kuanza kuwafundisha neno!!

NUNUA MAFUTA UPATE URODA (SEX)

Jamaa mmoja alikuwa anaendesha gari mitaa ya mjini kati na kukutana na bango kubwa (tangazo) lililoandikwa 

"Nunua mafuta ya gari yako na pata uroda (sex) bure".

Jamaa kwa kiwewe akakata kulia na kwenda katika kituo cha mafuta alichoelekezwa. Baada ya kujaza mafuta akamuuliza muhudumu 


"vipi kuhusu uroda wa bure?"

bila kuchelewa muhudumu huyo(mwanaume) akampa lundo la tiketi na kumtaka achague moja.

Jamaa akachagua namba 3 na kumpa muhudumu. Muhudumu akaiangalia na kumwambia 

'umekosa, jaribu siku nyingine". 

Kwa muda wa mwezi mzima jamaa akawa anapitia katika kituo hicho cha mafuta na kujaribu bahati yake; hata hivyo hakupata kitu.

Mwisho jamaa akakasirika na kumwambia muhudumu, 


"nyie matapeli sana, mwezi huu kila siku nimekuwa nikija kujaza petrol katika kituo hiki, lakini
sijafanikiwa kupata uroda wa bure...inaelekea nyie ni wasanii tu"

Mhudumu akamwambia 


"sie sio wasanii, inategemea na bahati ya mtu, kama huamini nenda kamuulize mkeo maana yeye mwezi huu tu ameshashinda mara Kumi na mbili !!"