Saturday, May 17, 2014

NUNUA MAFUTA UPATE URODA (SEX)

Jamaa mmoja alikuwa anaendesha gari mitaa ya mjini kati na kukutana na bango kubwa (tangazo) lililoandikwa 

"Nunua mafuta ya gari yako na pata uroda (sex) bure".

Jamaa kwa kiwewe akakata kulia na kwenda katika kituo cha mafuta alichoelekezwa. Baada ya kujaza mafuta akamuuliza muhudumu 


"vipi kuhusu uroda wa bure?"

bila kuchelewa muhudumu huyo(mwanaume) akampa lundo la tiketi na kumtaka achague moja.

Jamaa akachagua namba 3 na kumpa muhudumu. Muhudumu akaiangalia na kumwambia 

'umekosa, jaribu siku nyingine". 

Kwa muda wa mwezi mzima jamaa akawa anapitia katika kituo hicho cha mafuta na kujaribu bahati yake; hata hivyo hakupata kitu.

Mwisho jamaa akakasirika na kumwambia muhudumu, 


"nyie matapeli sana, mwezi huu kila siku nimekuwa nikija kujaza petrol katika kituo hiki, lakini
sijafanikiwa kupata uroda wa bure...inaelekea nyie ni wasanii tu"

Mhudumu akamwambia 


"sie sio wasanii, inategemea na bahati ya mtu, kama huamini nenda kamuulize mkeo maana yeye mwezi huu tu ameshashinda mara Kumi na mbili !!"

No comments:

Post a Comment