Wednesday, May 9, 2012

BONGE YA MTU KAINGIA BAR...



Jamaa bonge ya mtu...baunsa.... kaingia Bar;

Jamaa:
"Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji."*beer*

Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,

Jamaa:
"Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu."

Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi

Jamaa:
"Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake."

Raia kama kawa walitamani kumrukia ila kucheki mwili wakanywea....

No comments:

Post a Comment