Tuesday, May 8, 2012

DAH HUYU MTATA TUMFANYEJE???...


Devi kamwona mwenzie waliesoma nae siku nyingi akiwa amejiinamia kwa 


masikitiko kwenye baa. Akamsogelea,




Devi: Aise Abuu, habari za siku nyingi?



Abuu: Safi japo si safi sana, nina mawazo sana, maisha yamekuwa magumu sana 


ndugu yangu.



Devi: Nini tatizo unaonekana uko hovyo sana



Abuu: Niko hovyo ndugu yangu. Unajua Mzee wangu alifariki mwaka jana 



Januari, akaniachia urithi wa shilingi milioni sita. Miezi mitano baadae, mama 


akafariki akaniachia nyumba nikauza nikapata milioni 22,



Devi: Duh aise pole sana kupoteza wazazi wote mfululizo lazima ikupe mtu 



mawazo.



Abuu: Mjomba nae baada ya miezi mitano kafariki akaniachia milioni 4




Devi: E bwanaee mbona mikosi? Kila miezi mitano unapoteza mtu?




Abuu: Mikosi kweli sasa imeshapita karibu miezi minane kimya na hela 



imeshaisha ndugu yangu

No comments:

Post a Comment