Tuesday, May 1, 2012

MKULIMA.....



MKULIMA mmoja alikuwa na shamba la matikiti maji sasa kukawa kuna watoto wanakuja wanamwibia matikiti yake akafikiria jinsi ya kupambana na wale watoto mwisho akapata wazo la kuandika tangazo lilikuwa linasomeka hivi

"TIKITI MOJA HUMU SHAMBANI LIMETIWA SUMU" 

....Wale watoto walipokuja wakaliona lile tangazo wakafikiria kisha na wao wakaandika chini ya lile tangazo la mwenye shamba.......!!
Yule mkulima alipokuja akakuta hakuna hata tikiti moja lililoibiwa akafurahi mara akaona tangazo la waliloandika wale watoto likisomeka

"SASA MATIKITI YENYE SUMU YAMEKUWA MAWILI

No comments:

Post a Comment