Thursday, February 28, 2013

NGOJA NKUKUTE...!!!

Siku moja jamaa si kamdanganya mke wake eti anaenda safari kikazi Arusha, akachukua tax kazunguka mjini kumbe anahamia kwa kimada nyumba ya pili toka kwake. 

Unajua kilichoendelea?

Asubuhi yake jamaa akachungulia kwa kupitia dirishani kwa kimada ili aangalie kwake hali inaendeleaje, akamwona jamaa anapiga mswaki huku kajifunga taulo lake bila wasiwasi wote. 

Akapiga kelele: 

nani wewe? 

Jamaa akajibu: 

mambo ya mjini bwana, huyu mume wake kaenda kikazi Arusha kwa hiyo mimi ndo nipo hapa najipumzisha. 

Kwa hasira mwenye mke akajibu: 

we ngoja nikukute nikirudi kutoka Arusha!!

No comments:

Post a Comment